alimkabili mumewe na kumuuliza mwanamke huyo ni nani.
Mwanamume Mhindi alitua matatani na Idara ya Magari ya Kerala na mkewe baada ya kamera za usalama barabarani kuonekana kumuweka wazi.
Alionekana akisafiri kwa skuta yake huko Thiruvananthapuram bila kofia, ambayo ni ukiukaji wa trafiki.
Hata hivyo mwanamume huyo ambaye jina lake halikutajwa pia alionekana akisafiri na mwanamke jambo lililomfanya mkewe kushuku kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Mnamo Aprili 25, 2023, mwanamume huyo alikiuka sheria ya trafiki wakati kamera za AI zilipomnasa akisafiri na mwanamke huyo.
Kwa sababu mkewe ndiye aliyekuwa mmiliki wa gari hilo, maelezo ya ukiukaji wa sheria za barabarani yalitumwa kwake kupitia ujumbe mfupi wa maandishi.
Maelezo yalijumuisha sheria iliyovunjwa, picha ya skuta na faini iliyohitajika kulipwa.
Mwanamke huyo alipopokea ujumbe huo, alimkabili mume wake na kumuuliza mwanamke huyo ni nani.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32 alidai kuwa hakuwa na uhusiano na mwanamke huyo na kusema kwamba alikuwa tu rafiki ambaye alikuwa akimpa lifti.
Hata hivyo, mkewe hakuamini na alishuku kwamba alikuwa akimlaghai.
Hii ilisababisha ugomvi kati ya wanandoa.
Mnamo Mei 5, 2023, aliwasilisha malalamishi katika Kituo cha Polisi cha Karamana, akidai kuwa mumewe alimdhulumu yeye na mtoto wao wa miaka mitatu.
Ingawa hakuna ushahidi uliopatikana hadi sasa, kesi iliwasilishwa kulingana na taarifa hiyo.
Mtu huyo alikamatwa baadaye.
Afisa wa polisi alisema: "Aliwekwa chini ya ulinzi kulingana na maelezo yake. Kukamatwa kulirekodiwa chini ya IPC 321 (kusababisha madhara kwa hiari), 341 (vizuizi visivyofaa) na 294 (vitendo vichafu) na Kifungu cha 75 cha Sheria ya Haki ya Watoto (kushambulia au kutelekeza mtoto)."
Afisa huyo aliendelea kusema kuwa mwanamume huyo alifikishwa mbele ya mahakama. Baadaye alirudishwa rumande.
Licha ya kunaswa kwenye kamera na mwanamke mwingine, haijulikani ikiwa kweli alikuwa mpenzi wake.
Wakati huo huo, jimbo la Kerala limekuwa likishuhudia mzozo mkubwa wa kisiasa kuhusu uwekaji wa kamera kwenye barabara za serikali kama sehemu ya mradi wa usalama barabarani 'Safe Kerala'.
Chama cha upinzani cha Congress kilidai kuwa kulikuwa na dosari katika utekelezaji wa mfumo wa kamera wa AI.
CPI(M) ilikataa madai yote, na kuyaita "yasiyo na msingi".
Katibu wa Jimbo, MV Govindan alisema madai hayo yalitolewa ili kugeuza umakini kutoka kwa mafanikio ya serikali ya Kushoto.